Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Ali Akbar Velayati katika ukurasa wake binafsi kwenye mtandao wa X, akiwa ameambatanisha alama za reli #Iraq #Yemen #Lebanon, aliandika.
“Kuanza kwa kusitishwa mapigano huko Ghaza kunaweza kuwa nyuma ya pazia la kumalizika kwa kusitishwa mapigano mahali pengine.”
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Hamas mnamo tarehe 10 Oktoba ilitoa tamko ikitangaza kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kufuatia mazungumzo yaliyofanyika huko Sharm el-Sheikh.
Katika taarifa yake, Hamas ilisema:
“Baada ya mazungumzo yenye uwajibikaji na umakini yaliyofanywa na harakati pamoja na makundi ya mapambano ya Palestina kuhusu mapendekezo ya Rais wa Marekani huko Sharm el-Sheikh, yaliyolenga kumaliza vita na mauaji ya kimbari dhidi ya wananchi wa Palestina na kuwalazimisha wavamizi kuondoka katika Ukanda wa Ghaza, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina inatangaza kufikiwa kwa makubaliano yanayojumuisha kumaliza vita dhidi ya Ghaza, kuondoka kwa wavamizi, kuingizwa kwa misaada ya kibinadamu, na kubadilishana wafungwa.”
Your Comment